Shirika la Haki Afrika lalenga kwenda kortini kuhusu utata wa ardhi katika kaunti ya Lamu

  • | Citizen TV
    441 views

    Shirika la Kutetea Haki za Kibinaadam la HAKI AFRIKA linalenga kwenda mahakamani kufuatia utata wa ardhi inayodaiwa kuwa sehemu ya wavuvi wa fuo za bahari katika kisiwa cha Amu kaunti ya Lamu. Ardhi hiyo yenye ekari moja unusu kwa sasa inamilikiwa na mtu binafsi ambaye sasa anaendeleza ujenzi wa hospitali.