Strathmore yailaza Wakanda 38-19 kwenye mchuano wa ligi ya handiboli

  • | Citizen TV
    368 views

    Timu ya handiboli ya chuo kikuu cha Strathmore kilipata ushindi mkubwa wa magoli 19-38 dhidi ya timu ya wakanda kwenye mechi ya ligi kuu iliyochezwa siku ya jumapili katika uwanja wa nyayo. Kwenye mechi ya akina dada, amazon na nys zilitoka sare ya magoli 30-30 baada ya kutoka sare ya magoli 18-18 kufikia wakati wa mapumziko. Sylvia matere alikuwa mchezaji nyota wa nys baada ya kufunga magoli kumi. Kwa upande wa amazon, christine mwirigi alifunga magoli 11 naye rose anyango akaongeza magoli 10. Wachezaji wengine wanne walifunga magoli tatu na mbili.