Tanzania: Mkutano wa mfumo wa chakula wahimiza uwezeshaji wa wanawake

  • | VOA Swahili
    2,754 views
    Katika mkutano wa mfumo wa chakula na kilimo unaoendelea nchini Tanzania wadau wamehimizwa uwezeshaji wa wanawake katika kilimo, uvuvi na ufugaji ili kuongeza mchango wao katika kuimarisha mfumo wa chakula barani Afrika. Viongozi wa Afrika wapendekeza kuwepo na kodi mpya ya dunia na mageuzi katika taasisi za kimataifa za kifedha kwa ajili ya kusaidia kuchukuliwa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C. #habari #voaswahili #mkutano #mifumo #kilimo #chakula #tanzania #wadau #wanawake #mageuzi #taasisi #kimataifa #kifedha #voa #voaswahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.