Waziri wa Huduma za Umma na Jinsia Jumwa ahutubia kongamano la kumi na tatu la Jumuia ya Madola

  • | Citizen TV
    448 views

    Waziri wa Huduma za Umma na Jinsia, Aisha Jumwa leo amehutubia kongamano la kumi na tatu la jumuia ya madola. Waziri Jumwa kupitia mawasiliano ya kidijitali akiwa hapa nchini kenya amewasilisha ujumbe wa taifa kwa wajumbe walioko nchini Bahamas kwa kongamno hilo. Aidha amejadili masuala ya kuimarisha masuala yanayofungamana na wanawake ulimwenguni ikiwa ni pamoja na uongozi, mikakati ya kukabiliana na dhulma za kijinsia, uwekezaji miongoni mwa wanawake na athari za mabadiliko ya tabia nchini kwa mmanufaa ya wanawake ulimwenguni.