Rais Ruto aahidi kukuza sanaa na talanta za vijana

  • | Citizen TV
    426 views

    Washindi wa tamasha za kitaifa za muziki wamekongamana katika ikulu ndogo ya rais ya Nakuru ili kumtumbuiza Rais William Ruto pamoja na viongozi wengine wa kitaifa. Wanafunzi wa shule tofauti kote nchini waliobobea katika tamasha za muziki zilizokamilika mjini Nakuru wanapata fursa adimu ya kutangamana na kumtumbuiza rais. Rais amepongeza washindi wa mwaka huu huku akiahidi kuwa serikali yake itahakikisha inakuza talanta za wasanii wa sanaa ya aina zote nchini.