Waziri wa Usalama Kindiki awaonya maafisa wafisadi katika jumba la Nyayo

  • | Citizen TV
    255 views

    Waziri wa Usalama Profesa Kithure Kindiki amesema kuwa ufisadi katika idara ya Uhamiaji inachangia kukithiri kwa uhalifu na ugaidi nchini. Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya bunge, Kindiki amesema kuwa jumba la Nyayo lililoko hapa jijini Nairobi ni kitovu cha ufisadi huku akiahidi kuwa atakomesha utepetevu na ulaji rushwa katika jumba hilo. Aidha watu 58,000 bado wanasubiri kupata pasi za usafiri zinazofaa kutolewa baada ya siku saba pekee.