Wadau wa sekta ya uvuvi mjini Malindi wamefanya maandamano ya amani katika kituo cha kupokea samaki cha Shella wakipinga mswada wa usimamizi na maendeleo ya uvuvi wakisema unakiuka katiba, na unalenga kumkandamiza.
Wadau hao wakiongozwa na maafisa wa BMU, wakiwemo wavuvi Pamoja na wauzaji samaki wanasema kuwa serikali kupitia taasisi zinazohusika na uvuvi na masuala ya baharini hazikufanya ushirikishwaji wa umma kupata maoni kutoka mashinani wakishinikiza kufutiliwa mbali kwa mswada huo. Miongoni mwa sheria zilizopendekezwa ni kutozwa ada ya zaidi ya shilingi elfu 7 kwa mwaka kwa wamiliki wa boti ndogo za uvuvi.