Siku chache baada ya Rais William Ruto kuhakikishia ujumbe maalum kutoka Kisii uliozuru Ikulu kuhusu ujenzi wa barabara kadhaa eneo la Gusii,
Wakurugenzi wakuu kutoka mamlaka za ujenzi wa Barabara nchini KURA na KeNHA wamezuru Kisii kukagua jinsi miradi hiyo ya barabara itakaavyoazishwa.
Wakihutubia wanahabari katika uga wa Gusii wakiongozwa na gavana wa kaunti hiyo Simba Arati, barabara kutoka Daraja Mbili hadi Daraja Moja ( Fly over) ni miongoni mwa miundo msingi inayotarajiwa kujengwa Kisii karibuni.