Kampuni ya teknolojia Boston imetengeneza mkono wa bandia unaoweza kuzungumza lugha ya ishara

  • | VOA Swahili
    27 views
    Kampuni ya teknolojia iliyoko Boston imetengeneza mkono wa bandia ambao unaweza kuzungumza lugha ya ishara. Umekusudiwa kwa ajili ya watumiaji wasioona na kusikia, mkono huo unatafsiri maandishi ya mtandaoni kwenda katika lugha ya alama. Walioutengeneza wanasema una uwezo wa kufungua ulimwengu maudhui ya kidigitali kwa watumiaji wasioona na kusikia. Hii ni hiyo Tatum T1 Mkono wenye Vidole vyenye kutamka herufi “Tatum Robotics ni kampuni ya teknolojia saidizi yenye makao yake Boston, na lengo letu ni kutengeneza nyenzo ya kwanza saidizi ya mawasiliano kwa ajili ya jamii ya watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia ambao wanaweka kipaumbele matumizi ya alama. “Hivyo watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia wanawasiliana kupitia alama, pia zinajulikana kama alama ya mkono juu ya mkono mwengine.” Hivyo basi mtu mwenye ulemavu wa kusikia kuona huushika mkono kwa nyuma na hupokea alama katika kiganja chake moja kwa moja.” T1 imechukua nafasi ya mkono wa mtu kutafsiri maandishi yaliyoko katika mtandao. “Nitachapa neno hapa kujaribu – Nitaandika neno na kisha nitaliwasilisha na baadae Jaimi atanieleza hiyo alama inamaana gani.” //”S-n-a-i-l, yep, yep, hivyo neno nililoandika lilikuwa “snail’.” Roboti huyo anaweza kutumiwa nyumbani na mashuleni kutafsiri barua pepe, tovuti, na vitabu vya mitandaoni na zaidi. “Hivi sasa, mtu mwenye ulemavu wa kuona na kusikia nyumbani, wengi wao wanatengwa sana.” “Kwa kweli tunataka kuhakikisha kuwa watu wanaweza kufikia habari, huduma za afya, elimu, jamii yao, bila ya utegemezi kama vile watu wengine wanaosikia na kuona wanavyoweza kutumia fursa mbalimbali hivi leo.” #kampuni #teknolojia #boston #mkono #TatumRobotics #mkono #bandia #tafsiri #habari #hudumayaafya #elimu #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.