Baraza la magavana lakosoa waziri Nakhumicha kuhusiana na miswada ya afya ilioko bungeni

  • | Citizen TV
    597 views

    Baraza la magavana limemkosoa Waziri wa afya susan nakhumicha kwa kuwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu afya bila kuwahusisha. magavana wanasema kuwa baadhi ya vipengee ambavyo vinahusu ukusanyaji wa fedha za hazina ya matibabu, uwazi wa data za wakenya walioko chini ya mpango huo na gharama kwa serikali za kaunti vina utata. aidha waziri nakhumicha amewahakikishia magavana kuwa kila mmoja atapata data kuhusu kaunti yake huku akisisitiza kuwa miswada hiyo ilitokana na ripoti zilizoko.