Kongamano la sukari lafanyika Kakamega

  • | Citizen TV
    299 views

    Kaunti za ukanda wa ziwa na zingine ambazo hukuza miwa zinakongamana mjini kakamega kutafuta suluhisho kwa matatizo yanayowazonga wakulima wa miwa.. Gavana wa kakamega fernandes Barasa ambaye ni mwenyeji wa kongamano hilo anasema kwamba serikali za kaunti na ile ya kitaifa zitashirikiana kuhakikisha kwamba wakulima wanapata faida kutokana na jasho lao. sekta ya sukari imekabiliwa na mzigo wa madeni huku kampuni za sukari zikifunga kazi kutokana na kupungua kwa kiwango cha miwa. baadhi ya wakulima wamekuwa wakiwasilisha miwa ambayo haijakomaa, hali ambayo imechangia hali hiyo. serikali imeahidi kufufua viwanda vya sukari eneo la magharibi.