Washukiwa 10 akiwemo afisa wa DCI wakamatwa Nairobi kwa tuhuma za utapeli wa dhahabu ghushi

  • | Citizen TV
    9,117 views

    Washukiwa 10 akiwemo afisa wa DCI wamekamatwa jijini Nairobi kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli wa dhahabu ghushi. Katika operesheni hiyo iliyoanza alhamisi juma lililopita wapelelezi wa DCI wamemnasua raiya mmoja wa kigeni katika mtego wa kumlaghai shilingi bilioni moja. Hassan Mugambi anaarifu kuwa matapeli hawa wamekuwa wakilindwa na baadhi ya wanasiasa na maafisa wa polisi wa ngazi za juu.