Libya: Watu wasiopungua 2,000 wafariki, zaidi ya 10,000 hawajulikani waliko

  • | VOA Swahili
    511 views
    Picha za video zikionyesha ukubwa wa mafuriko nchini Libya zilisambazwa na huduma za dharura za mji ulioko kaskazini mashariki wa Bayda Jumanne. Kiasi cha watu 50 wameripotiwa kuwa wamepoteza maisha katika mji huo. Mamlaka nchini Libya Jumanne zilisema kuwa watu wasiopungua 2,000 wamefariki na maelfu hawajulikani walipo katika kufuatia janga la mafuriko lililolikumba taifa la Afrika Magharibi Jumapili, huku likiharibu barabara kadhaa na majengo. Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Mwezi Mwekundu, IFRC, ilisema “ vyanzo vyao vyakujitegemea vya habari” vilithibitisha kuwa “idadi ya watu waliotoweka imefikia 10,000 hivi sasa.” - AP / VOA #Libya #RedCross #RedCrescent - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.