Skip to main content
Skip to main content

Wananchi walalamikia mienendo ya Polisi

  • | Citizen TV
    3,483 views
    Duration: 3:01
    Maafisa wakuu wa usalama nchini , wakiwemo waziri wa usalama wa ndani na katibu mkuu wa wizara hiyo, waliwekwa kwenye mizani kuhusu kuzorota kwa imani kati ya wananchi na maafisa wa polisi. Ni hali iliyojitokeza wazi wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu hali ya usalama nchini, ambapo wananchi walieleza wasiwasi wao kuhusu mienendo ya polisi katika matukio ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa imani ya wananchi. Waziri wa usalama wa ndani, Kipchumba Murkomen, alipokuwa akijibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi, aliwatetea polisi huku akielekeza lawama kwa wanasiasa, akiwashutumu kwa kuchochea matatizo yanayodhoofisha imani ya wakenya dihidi ya taasisi za usalama.