Sababu za Chiloba kusimamishwa kazi zaanikwa

  • | K24 Video
    47 views

    Imebainika kuwa Ezra Chiloba ambaye amesimamishwa kazi kama mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini huenda amehusika katika ubadhirifu wa shilingi milioni mia sita sitini na mbili kupitia mikopo ya kununua nyumba na ardhi. Kulingana na ripoti ya bodi maalum ya ukaguzi iliyomulika mamlaka hiyo, Chiloba amehusishwa na sakata hiyo kwa tukio la shilingi milioni ishirini na tano kulipwa kwa kampuni yake baada ya kujiidhinishia kununua nyumba. Aidha anadaiwa kununua ekari saba za shamba badala ya moja pekee kama inavyohitajika. mwanahabari wetu joel chacha na taarifa hiyo.