Huenda serikali ikashindwa kutimiza ahadi zake

  • | Citizen TV
    2,446 views

    Huenda serikali ikashindwa kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo kutokana na uhaba wa fedha. Haya ni kwa mujibu wa msimamizi wa bajeti Margaret Nyakango ambaye ameonya kuwa, Kenya kwa sasa imepita kiwango kilichowekwa kulipia madeni, ambayo kwa sasa ni zaidi ya shilingi trilioni 10. Nyakango akisema. Asilimia 83 ya fedha zinazokusanywa na serikali kwa sasa zinatumika kulipia madeni ya serikali.