Muungano wa wauguzi Nyamira yatoa ilani

  • | Citizen TV
    243 views

    Muungano wa wauguzi katika kaunti ya Nyamira wametoa ilani ya siku 14 ya kufanya mgomo iwapo serikali ya kaunti hiyo haitatatua matakwa yao. Viongozi wa muungano huo wameelezea masikitiko yao kufuatia kutopandishwa vyeo kwa wanachama wao huku mishahara ya baadhi yao ikikosa kuidhinishwa hata baada ya kupandishwa vyeo. pia wanalalamikia kucheleweshwa Kwa mishahara na marupurupu, na kukatwa ada ya masomo kwa wanachama waliogharamia masomo yao binafsi.