- 302 viewsDuration: 1:32Mamlaka ya IPOA leo imezindua sera ya kufanyia mabadiliko idara ya polisi huku idara hiyo ikipewa taarifa mchanganyiko kuhusiana na utendakazi wa maafisa wa usalama. Suala la haki miongoni mwa waathiriwa ambapo wamekabiliwa na polisi pia lilipewa kipaumbele. Aidha pendekezo la kutoa fidia kwa waathiriwa wa maandamano limejadiliwa lakini wasemaji wamesisitiza kuwa lazima kuwe na haki ambapo polisi wahusika wanakabiliwa kisheria.