Boaz Ombewa apuuzilia mbali ombi la wakili kutaka afisi ya mashtaka ya umma kupunguza mashtaka

  • | KBC Video
    9 views

    Washukiwa 12 wanaotuhumiwa kwa wizi katika chama cha ushirika cha Njiwa cha shirika la huduma ya kitaifa ya ujasusi watazuiliwa kwa siku 21 katika gereza la wanawake la Lang’ata na lile la Kiambu. Akitoa uamuzi huo katika mahakama ya Kahawa hakimu mkuu mwandamizi Boaz Ombewa alipuuzilia mbali ombi la wakili wa upinzani la kutaka afisi ya mashtaka ya umma kupunguza mashtaka yanayowakabili washukiwa kutoka 223 hadi 12. Katika uamuzi wake, Ombewa alisema ombi hilo halingeruhusiwa na mahakama na kwamba kila mshukiwa atakiri au kukanusha mashtaka kibinafsi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channe: l: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive