Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei atoa onyo kali kwa maafisa wa polisi wanaoendeleza ufisadi

  • | Citizen TV
    2,991 views

    Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi wanaoendeleza ufisadi akiwaeleza kuwa watabeba msalaba wao wenyewe na si kikosi kizima. Katika kongamano lililowaleta pamoja maafisa wa ngazi za juu katika idara ya polisi, koskei ametoa wito kwa kila afisa kuweka taifa na mwananchi mbele katika utendakazi wake . Kwa upende wake inspekta mkuu wa polisi ameahidi kuwa hakuna anayejihusisha na ufisadi atakayesazwa na idara ya kuchunguza nidhamu ya polisi.