Wanafunzi 2,500 wa udaktari kurejelea masomo KUTRRH

  • | Citizen TV
    101 views

    Ni afueni kwa wanafunzi 2,500 wa somo la udaktari na uuguzi katika chuo kikuuu cha kenyatta baada ya bodi ya hospitali ya mafunzo na utafiti ya chuo kikuu cha kenyatta kuwaruhusu wanafunzi kupokea mafunzo katika hospitali hiyo. inaarifiwa kuwa wanafunzi wa chuo hicho wamekuwa wakipokea mafunzo katika chuo cha kiambu kwa miaka miwili kutokana na changamoto za fedha za hospitali ya chuo cha kenyatta ambayo ilisababisha ukosefu wa vifaa vinavyohitajika kwa mafunzo ya udaktari.