- 88 viewsDuration: 1:24Maaskofu na makasisi wa kanisa la Kianglikana tawi la Bungoma wametangaza kumuunga mkono Mbunge wa Westlands Timothy Wanyonyi katika azma yake ya kuwania ugavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi mkuu ujao. Wakiongozwa na mwenyekiti wao Askofu George Mechumo, wametangaza kuwa walichukua hatua hiyo baada ya kufanya udadisi miongoni mwa wagombea wote na kubaini kuwa Tim Wanyonyi ana sifa bora za uongozi kutokana na tajriba yake ya uongozi Nairobi.