Mahojiano na Mbunge wa Bunge la Israel Aida Touma-Suleiman

  • | VOA Swahili
    56 views
    “Nilipokuwa natoa hotuba yangu katika Bunge la Israel (Knesset) nilikuwa nasema watoto huko kusini mwa nchi hii na huko Gaza wanastahili kuishi na wakaanza kelele hizo na mimi, unaweza kuona kuwa nilipatwa na aina fulani ya mshtuko kwa muda mfupi. Ukweli, sikuweza kufikiria kuwa kuna mtu ataniambia kuwa hakuna usawa baina ya watoto hawa, na watoto hawako sawa. Hilo sawa. Iwapo unazungumzia kuhusu watu wazima, simaanishi kuwa hilo linakubalika, lakini tunaweza kubishana. Lakini watoto? Watoto wasio na hatia? Na kuna mtu anahoji haki za watoto kuishi? Halafu limekuja jambo baya sana, kwa maoni yangu , ni hukumu ambayo kwa jumla imenishtua sana kwamba watoto wa Gaza wamejisababishia wato wenye, ikimaanisha kupigwa mabomu na kuuwawa. Hakuna maelezo. Ninaweza kulia kwa ajili ya Myahudi, Mhindu au mtoto mwengine ambaye ameuawa kama nitakavyo mlilia mtoto wa Kipalestina, ambaye ameuawa. #israel #gaza #iran #reels #igreels #voa #voaafrica #knesset #hadash