Daktari asambaza video ikionyesha msongamano hospitalini watu waliojeruhiwa

  • | VOA Swahili
    424 views
    Daktari mmoja katika hospitali huko Gaza amesambaza kanda ya video inayoonyesha sehemu zilizojaa msongamano wa watu waliojeruhiwa huku vita vya sasa kati ya Israel na Hamas vikiendelea. Video hiyo, ilichukuliwa Ijumaa iliyopita, iliwaonyesha wagonjwa, waliokuwa wamefanyiwa upasuaji, wakiwa wamesimama katika maeneo mbalimbali ya Hospital ya Shifa huko Gaza City. Katika moja ya picha hizo, mtu mmoja anaonekana akiwa amelala kwenye kitanda kilicho tapakaa damu. Dkt. Marwan Abusada, ambaye ni mkuu wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Shifa, alisema kuwa hospitali hiyo ilikuwa imeelemewa na wagonjwa na kulikuwa hakuna chumba kupokea wagonjwa wapya. Shifa is one of the main hospitals in the northern half of the Gaza Strip. Shifa ni moja ya hospitali kadhaa kuu katika nusu ya upande wa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesihi kuwepo na sitisho la haraka la mapigano ili kuruhusu misaada kuingia katika eneo la Wapalestina, wakati chakula, maji na mafuta yanayohitajika kwa ajili ya majenereta yanayotoa umeme hospitalini yakiwa yanakwisha. (AP) #israel #gaza #iran #reels #igreels #voa #hamas