- 3,993 viewsDuration: 1:47Rais William Ruto amemkosoa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akisema anawapotosha wakazi wa Ukambani kuhusu maswala ya uongozi bora na maendeleo. Rais ambaye alihudhuria ibada maalum katika chuo cha Eastern Kenya Intergrrated College eneo la Mitaboni, kaunti ya Machakos, aliwarai wakazi wa eneo hilo kuunga mkono jitihada zake za kuunganisha jamii zote nchini ili kuleta usawa na maendeleo. Rais Ruto ambaye alipokewa na waziri wa Leba Dkt. Alfred Mutua, aliwakashifu viongozi wa upinzani akisema wanaeneza siasa za chuki na mgawanyiko. Hata hivyo amesema kuwa hatatenga maeneo yanayoongozwa na viongozi wa upinzani kimaendeleo.