Juhudi za kukomesha matumizi ya plastiki duniani zaenelea

  • | VOA Swahili
    38 views
    Juhudi za kutengeneza mkataba wa kihistoria wa kukomesha matumizi ya plastiki duniani zinaendelea katika mji mkuu wa Kenya ambapo mataifa, makampuni, wanamazingira na waathirika wa uchafuzi wa mazingira wamekusanyika ili kujadili matumizi ya plastiki. Mkutano huo mjini Nairobi ni wa tatu katika ratiba ya mikutano mitano inayonuiwa kukamilisha mazungumzo mwishoni mwa mwaka ujao. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.