Helikopta za umeme kutumika kusafirisha abiria kutoka uwanja wa ndege New York

  • | VOA Swahili
    389 views
    Meya wa jiji kuu la bishara la Marekani New York, Eric Adams amesema, katika kipindi cha karibu miaka miwili abiria kutoka mashirika ya ndege watasafirishwa kwa helikopta zinazotumia umeme kutoka uwanja wa ndege hadi katikati ya jiji. Usafiri huo utawawezesha kuepukana na msongamano wa magari na kupunguza matumizi ya mafuta yanayochafua mazingira. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.