- 3,507 viewsDuration: 45sRais william ruto amewasili nchini marekani kuhudhuria kikao cha themanini cha baraza kuu la umoja wa mataifa - unga. Kikao hiki huwaleta pamoja marais wa mataifa mbali mbali kuhudhuria na pia kuhutubia wajumbe kuhusu hali ya mataifa yao na ulimwengu kwa jumla. Rais ruto anatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu hali ya kifedha duniani, usawa katika utoaji wa mikopo kutoka mataifa yaliostawi na vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Rais ruto pia atashauriana moja kwa moja na baadhi ya marais na wakuu wa sekta binafsi duniani ili kuimarisha uhusiano na pia kutafuta fursa mpya za uwekezaji.