- 4 viewsKampuni ya kusambaza maji ya Garissa GAWASCO, imetoa ilani kwa wateja wake kuwa kutakuwa na uhaba wa maji katika mji huo kutokana na ujenzi wa daraja katika barabara kuu ya Garissa kuelekea Nairobi. Akizingumza na waandishi wa habari, afisa wa uhusiano mwema wa kampuni hiyo Omar Abdullahi alisema ujenzi huo umebadili mkondo wa maji kwenye mto Tana na hivyo kupunguza kiasi cha maji cha kila siku kwenye mtambo wao wa kusafisha maji.