Skip to main content
Skip to main content

Tume ya EACC yachunguza ajira za watu zaidi Siaya

  • | Citizen TV
    173 views
    Duration: 1:54
    Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC imeanza rasmi uchunguzi kuhusu madai ya uajiri wa madaktari mia tano katika kaunti ya Siaya. Kulingana na mkurugenzi wa tume hiyo ukanda ya Magharibi Abraham Kemboi, serikali ya kaunti ilitangaza nafasi mia moja za ajira katika sekta ya afya mwaka 2023, ila bodi ya umma ya kaunti hiyo ilitoa barua zaidi ya mia tano. Kemboi akisema kuwa hulka hiyo imeripotiwa katika sehemu mbalimbali ambapo baadhi ya maafisa wa kaunti wanakula mlungula na kutoa barua za ajira kinyume na sheria. Seneta wa Siaya Oburu Odinga pia alikuwa ametoa onyo kuhusu uajiri huo akiapa kuwaslisha suala hilo katika bunge la seneti ili kupiga msasa utendakazi wa serikali ya kaunti ya Siaya