Mamia ya wanafunzi wenye umri wa chini kutoka familia zenye uhitaji wakosa ufadhili wa masomo

  • | Citizen TV
    639 views

    Mamia ya wanafunzi wenye umri wa chini kutoka kwa familia zenye uhitaji walikosa ufadhili na ufadhili wa serikali kwa sababu ya kuwa na umri mdogo. Wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini bado hawajastahiki usaidizi wa serikali hadi watakapopata vitambulisho vyao. Wanafunzi hao ambao wengi awakuweza kuandika mitihani yao ya mwisho wa muhula kutokana na mabaki ya karo wanaituhumu serikali kwa kuvunja ahadi yake kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa ufadhili wa serikali Lakini kama Mary Muoki anavyoripoti, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Charles Ringera hata hivyo anasema bodi ilipokea maombi 26,000 ya mkopo kutoka kwa waombaji wenye umri mdogo na wote wamepokea ufadhili wao wa masomo, isipokuwa kesi chache ambazo wanashughulikia kutatua.