- 654 viewsRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametishia kutangaza vita dhidi ya Rwanda Jumatatu wakati wa mkutano wake wa mwisho wa kampeni za uchaguzi mjini Kinshasa. Akizungumza mbele ya maelfu ya wafuasi wake, Tshisekedi alisema “ikitokana na risasi ya kwanza iliyofyatuliwa, nitaitisha kikao cha bunge kwa sababu katiba inaniruhusu mimi kufanya hivyo, na nitatangaza vita dhidi ya Rwanda.” Wanasiasa wa Congo na makundi mbalimbali likiwemo la waasi wa M23, ambao wameteka eneo la mashariki mwa DRC, na Corneille Nangaa, mkuu wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Congo, walizindua ushirika wa Congo River Alliance huko Nairobi, Kenya Ijumaa. Nangaa, ambaye aliwekewa vikwazo na Marekani kwa ufisadi na kuingilia uchaguzi wa 2018, alisema muungano huo utavileta pamoja vikundi mbalimbali venye silaha vya Wakongo, wanamgambo, na jumuiya za kijamii na kisiasa. Hali ya kutokuwepo usalama ni sehemu ya athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa havijatafutiwa ufumbuzi ambavyo vilimalizika rasmi mwaka 2003. Mashambulizi ya hivi karibuni ya M23 yamechochea mivutano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Rwanda, ambapo DRC na wataalam wa UN wanaishutumu kwa kuwaunga mkono wanamgambo hao. Rwanda inakanusha kuhusika. Tshisekedi anachuana na takriban darzeni mbili za wapinzani katika uchaguzi mkuu siku ya Jumatano, Disemba 20. Wapinzani wake ni pamoja na hasimu wa kisiasa wa zamani kama Martin Fayulu, ambaye alitwaa nafasi ya pili katika uchaguzi uliokuwa na utata wa 2018, na mshindani mwengine ni Mshindi wa Tuzo ya Nobel Dr. Denis Mukwege. #drc #rwanda #congo #felixtshisekedi #tshisekedi #drcelection #drcelection2023 #voa
Tshisekedi Atishia kutangaza vita dhidi ya Rwanda katika kampeni ya mwisho
- 16 Aug 2025 - President William Ruto is scheduled to tour the United States next month for the 80th session of the United Nations General Assembly (UNGA) in New York, marking his first trip to the U.S. under President Donald Trump’s administration.
- 16 Aug 2025 - The killer Coptic roundabout in Mamboleo along Kisumu Kakamega highway has been dug out by unknown people last night following cases of road accidents in the area, with the latest claiming 27 lives, out of which 22 are set to be laid to rest today in…
- 16 Aug 2025 - The Democratic Republic of Congo (DRC) has raised objections over President William Ruto's nomination of a new Consul General to Goma, warning that such nominations require prior approval from Congolese authorities.
- 16 Aug 2025 - Politics can be messy, even desperate. But to cross the line into the indignification of women — reducing them to objects for male amusement — is not desperation. It is degradation.
- 16 Aug 2025 - The last days of July and the early weeks of August have been marked by a wave of
- 16 Aug 2025 - Kenya Power has issued a notice of planned power outages affecting parts of Nairobi, Machakos, Nakuru, and Mombasa
- 16 Aug 2025 - He described the voting process as irregular and predetermined.
- 16 Aug 2025 - Ghana international Semenyo took to Instagram after the game to show more racist abuse he had received.
- 16 Aug 2025 - Kipyegon clocked a blistering 8:07.04, the second-fastest time ever recorded over the distance
- 16 Aug 2025 - Deputy President Kithure Kindiki has warned opposition leaders against any attempts to destabilize the country to gain power, declaring such acts to be dangerous and unacceptable.