Washukiwa 250 wa kundi haramu la Mungiki wakamatwa

  • | K24 Video
    46 views

    Washukiwa 250 wa kundi haramu la Mungiki wamekamatwa huku magari 16 yakinaswa, kufuatia msako mkali wa polisi huko Nyeri dhidi ya mkutano uliokuwa umepangwa na aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga katika uwanja wa maonyesho wa Kabiruini kaunti ya Nyeri. Akidhibitisha kukamatwa kwao, naibu kamishna wa nyeri ya kati Joseph Mwangi amesema, washukiwa walikamatwa baada ya kupatikana na vifaa vinavyohusishwa na kundi hilo haramu ikiwemo tumbako, bendera za kundi miongoni mwa vifaa vingine. Washukiwa wanadaiwa kutoka kaunti mbali mbali ikiwemo, Nyeri, Muranga, Kiambu, Baringo, Kirinyaga na Laikipia.