- 2,063 viewsDuration: 3:15Familia ya Simon Warui, aliyefariki akiwa korokoroni katika kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa, imetofautiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wake ambao ulionyesha kuwa alifariki kwa kukosa pumzi baada ya kuvunjika shingo. Kwa mujibu wa polisi, Warui alianguka kutoka juu na kufariki. Hata hivyo, familia yake inadai njama ya kufichwa kwa ukweli kutoka kwa maafisa wa polisi.