- 2,702 viewsJeshi la Israeli limesema Jumatano wanajeshi wake ambao wamekuwa wakiendesha operesheni za kijeshi katika eneo la Khan Younis kwa siku kadhaa zilizopita wamegundua silaha mbalimbali, nyaraka za kijasusi na mahandaki. Hivi sasa Jeshi hilo linajikita katika operesheni kubwa mbalimbali huko kusini mwa mji wa Khan Younis na kambi za wakimbizi zilizoko katikati ya Gaza ambazo ziko tangu mwaka 1948 zikizunguka mahali Israel ilipoundwa. Mamia ya watu wameuawa katika siku za karibuni kutokana na mashambulizi yanayoendelea katika eneo lote hilo, ikiwemo maeneo ya mbali kusini ambapo watu waliambiwa waende kutafuta hifadhi. Tangu vita ilipoanza, mashambulizi ya Israel yameuwa zaidi ya Wapalestina 23,000, ikikadiriwa ni asilimia 1 ya idadi ya watu katika eneo hilo, na zaidi ya watu 58,000 wamejeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas. Takriban theluthi mbili ya waliofariki ni wanawake na watoto, maafisa wa afya wamesema. Idadi ya vifo haitofautishi kati ya wapiganaji na raia. Katika shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia. Waliwateka kiasi cha wengine 250, karibu nusu yao waliachiliwa huru katika kipindi cha wiki moja cha kusitishwa mapigano mwezi Novemba. #Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #khanyounis
Jeshi la Israeli likiendesha operesheni zake eneo la Khan Younis
- - FEASSA games day 2 ››
- - Consumer trends ››
- - Co-op Bank results ››
- 16 Aug 2025 - US President Donald Trump and Russian counterpart Vladimir Putin will meet on Friday in Alaska in a high-risk summit that could prove decisive for the future of Ukraine.
- 16 Aug 2025 - The Nairobi Hospital has announced the suspension of its recent price adjustments following consultations with key insurance partners, who had initially withdrawn their services, leaving patients stranded.
- 16 Aug 2025 - Homicide detectives on Friday returned to Kwa Binzaro in preparation for the planned exhumation of eight graves that had been discovered late last month.
- 15 Aug 2025 - Kericho Governor Erick Mutai has been impeached. The embattled Governor was ousted after putting up a spirited defense throughout the day before the County Assembly.
- 15 Aug 2025 - A group of youth from Jacaranda in Embakasi who attended last Saturday’s State House empowerment event claim they never received the promised motorbikes and other items.
- 15 Aug 2025 - Nairobi Senator Edwin Sifuna has challenged President William Ruto to name those he accused of soliciting money from Cabinet Secretaries and Governors, citing that such remarks require proof.
- » Kajiado girls betrayed at birth: Minors face Obstetric Violence, sky-high bills and brutal neglect15 Aug 2025 - Kajiado is marked as one of the counties where maternal and sexual reproductive health violations and obstetric violence cases are rampant.
- 15 Aug 2025 - The DP on Friday graced Tiaty Economic Empowerment engagement at Chemolingot town in the constituency where he avowed the rolling out of key projects geared at improving the lives of the residents.
- 15 Aug 2025 - Charity Nyambura, recently single, does not do butterflies
- 15 Aug 2025 - Videos seen by the Star showed members physically restraining one another while others exchanged harsh words