- 435 viewsDuration: 1:46Chama cha walimu wa Sekondari KUPPET kaunti ya Laikipia kimesisitiza umuhimu wa shule za JSS kujisimamia kikisema tofauti za viwango vya elimu kati ya wasimamizi wa shule za msingi na walimu wa JSS zinaleta mvutano mkubwa baina yao katika utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu CBE. Wakiongozwa na katibu wa chama hiki Laikipia Robert Miano, walimu hawa wanasema mgao wa fedha kwa mashule umekuwa ukielekezwa sana kwa shule za msingi na kuacha zile za JSS bila bidhaa muhimu