- 463 viewsMaelfu ya watu walikusanyika kufanya maombi ya kuachiliwa kwa mateka waliosalia wanaoendelea kushikiliwa Ukanda wa Gaza Jumatano mahali ulipo ukuta wa Western Wall Jerusalem. Eneo ambapo maombi yalifanyika Jumatano na umati wa watu ni sehemu takatifu sana kwa Wayahudi kufanya maombi. Hatma ya mateka hao inawatia wasiwasi Waisraeli na kuachiliwa kwao bado ni moja ya malengo ya serikali ya Israel katika vita yake dhidi ya Hamas. Katika shambulizi lao la Oktoba 7, Hamas na wanamgambo wengine waliwateka takriban watu 250, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto na wazee. Kiasi cha watu 110 wameachiliwa na wengine 110 wanashikiliwa, na huku watu 20 hivi ambao waliuawa wakiwa wanashikiliwa, mamlaka za Israeli zinasema. Mateka walioachiliwa wametoa maelezo ya kuhuzunisha walioshuhudia wakati wakishikiliwa, ambapo wengine walipewa chakula kidogo, kulazwa sakafuni na kuhofia maisha yao wakati wote huo. Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200. Mashambulizi ya Israel ya angani, ardhini na baharini huko Gaza yameuwa zaidi ya Watu 23,000, theluthi mbili kati ya hao ni wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas. Idadi hiyo haitofautishi kati ya raia na wanamgambo. - AP #Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #westernwall #mateka #jeshi
Israeli: Maelfu ya watu wakusanyika kufanya maombi ya kuachiliwa kwa mateka
- - FEASSA games day 2 ››
- - Consumer trends ››
- - Co-op Bank results ››
- 16 Aug 2025 - US President Donald Trump and Russian counterpart Vladimir Putin will meet on Friday in Alaska in a high-risk summit that could prove decisive for the future of Ukraine.
- 16 Aug 2025 - The Nairobi Hospital has announced the suspension of its recent price adjustments following consultations with key insurance partners, who had initially withdrawn their services, leaving patients stranded.
- 16 Aug 2025 - Homicide detectives on Friday returned to Kwa Binzaro in preparation for the planned exhumation of eight graves that had been discovered late last month.
- 15 Aug 2025 - Kericho Governor Erick Mutai has been impeached. The embattled Governor was ousted after putting up a spirited defense throughout the day before the County Assembly.
- 15 Aug 2025 - A group of youth from Jacaranda in Embakasi who attended last Saturday’s State House empowerment event claim they never received the promised motorbikes and other items.
- 15 Aug 2025 - Nairobi Senator Edwin Sifuna has challenged President William Ruto to name those he accused of soliciting money from Cabinet Secretaries and Governors, citing that such remarks require proof.
- » Kajiado girls betrayed at birth: Minors face Obstetric Violence, sky-high bills and brutal neglect15 Aug 2025 - Kajiado is marked as one of the counties where maternal and sexual reproductive health violations and obstetric violence cases are rampant.
- 15 Aug 2025 - The DP on Friday graced Tiaty Economic Empowerment engagement at Chemolingot town in the constituency where he avowed the rolling out of key projects geared at improving the lives of the residents.
- 15 Aug 2025 - Charity Nyambura, recently single, does not do butterflies
- 15 Aug 2025 - Videos seen by the Star showed members physically restraining one another while others exchanged harsh words