- 1,081 viewsDuration: 1:24Maafisa wa polisi eneo la Belgut kaunti ya Kericho wameanzisha uchunguzi wa kisa cha jamaa mmoja aliyewavamia watu watatu wa familia moja na kuwaua. Baada ya kutekeleza mauaji hayo, mshukiwa evans kiprono alishambuliwa na wenyeji na kuuawa. Kisa hiki kiliwaacha wenyeji vinywa wazi wasielewe ni vipi mshukiwa aliamua kutekeleza uhalifu kama huo. Polisi wanaarifu mshukiwa amekuwa akihusika na visa vya uhalifu aliwahi kufungwa jela. Miili ya waliouawa ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Kericho.