- 491 viewsDuration: 1:25Naibu rais Kithure Kindiki amewataka viongozi wa kaskazini mashariki kudumisha amani ili kufanikisha maendeleo eneo hilo. Akizungumza eneo la Irunduki kaunti ya Tharaka Nithi baada ya kukutana na zaidi ya wakaazi 1,500 kutoka kaunti ya Isiolo, Kindiki aliwataka wakaazi hawa kutangamana vyema ili kuhakikisha wanafikiwa na maendeleo kikamilifu. Aidha ameendelea kutoa hakikisho ya mikakati ya serikali kuhakikisha miundo msingi zaidi na maendeleo yanawafikia.