Viongozi wa Azimio wapinga pendekezo la mkutano wa Jaji mkuu na Rais

  • | K24 Video
    78 views

    Viongozi wa muungano wa Azimio wakiongozwa na kinara Raila Odinga wamepinga vikali hatua ya jaji mkuu Martha Koome kuitisha mkutano na rais William Ruto kufuatia mvutano wa mihimili miwili ya serikali kuhusiana na madai ya ufisadi yaliyoibuliwa na Ruto. Odinga na wenzake wameshikilia kuwa hatua hiyo itahujumu uhuru wa mahakama na hata kuathiri kesi zilizoko mbele ya korti.