Waziri Njeru atarajiwa kuzuru bwawa la Thwake huko Makueni

  • | Citizen TV
    482 views

    Waziri wa maji na miradi ya unyunyizaji maji mashamba Zachary Njeru anatarajiwa kuzuru mradi wa ujenzi wa bwawa la Thwake hii leo. Ziara hiyo ikiwa muhimu kwa wakaazi wa Makueni kuhusiana na mradi huo ambao umekumbwa na masaibu ya ukosefu wa fedha katika siku za hivi karibuni. Kampuni ya China Ghezouba ambayo ilipewa kandarasi hiyo wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikisitisha mradi huo mara kwa mara. Michael Mutinda anaarifu zaidi.