Wazee wa jamii za Wakuria, Wapokot, Wasamburu na Wasabaot wapania kumaliza ukeketaji kabisa

  • | Citizen TV
    219 views

    Kongamano la siku mbili la kujadili mikakati ya kukomesha ukeketaji limekamilika katika kaunti ya Samburu. Wazee kutoka jamii za Kuria, Pokot, Baringo, Sabaot na Samburu wakiafikiana kukomesha ukeketaji ifikapo mwaka alfu mbili na ishirini na tano. Hata hivyo imebainika kuwa kaunti za Kaskazini Mashariki zimesalia kuongoza kwa zaidi ya asilimia tisini ya visa hivyo.