Wanafunzi wa chuo kikuu cha MMU waandamana kulalamikia usalama wao dhidi ya mashambulizi ya fisi

  • | K24 Video
    63 views

    Wenyeji katika kijiji cha Olmeut huko Ongata Rongai Kajiado kaskazini wanaomboleza kifo cha mwana wao wanayesema alishambuliwa na fisi jana jioni alipokua akiokota kuni. Kisa hicho kikidaiwa kutokea wakati sawia na kile cha mwanafunzi wa chuo kikuu cha multimedia ambaye pia alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya na fisi jana usiku kijijini humo. Wanafunzi wa chuo hicho waliandamana mapema leo dhidi ya shirika la KWS wakitaka haki kwa mmoja wao aliyeathirika na ambaye sasa amelazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.