Kampuni zatakiwa ziongezee mishahara ya walinzi wa kibinafsi

  • | K24 Video
    188 views

    Zaidi ya walinzi wa kibinafsi na mabawabu laki saba huenda wakapoteza kazi zao iwapo ilani ya kisheria ya nyongeza ya mishahara itatekelezwa kikamilifu. Hayo ni kulingana na muungano wa kampuni zinazotoa huduma za ulinzi uliodai hautamudu gharama ya kuendesha biashara hiyo na hivyo wafanyikazi watapunguzwa. Haya yanajiri baada ya mamlaka ya kuangazia utendakazi wa walinzi kupokonya leseni kampuni tisa ambazo hazijatekeleza nyongeza ya mishahara ya walinzi.