Wakazi wa Samburu wasema kuhojiwa kwa viongozi hakusaidii mashambulizi kupunguka

  • | Citizen TV
    177 views

    Siku chache baada ya Gavana wa kaunti ya Samburu na viongozi wengine kuwa wageni wa maafisa wa upelelezi katika makao makuu ya upelelezi wa jinai jijini Nakuru, wakazi wa kaunti ya Samburu wameisuta idara hiyo kuwa licha ya kuwahoji viongozi kila mara mashambulizi yamesalia kuripotiwa Samburu. Wameitaka serikali kushirikiana na viongozi wanaotoka maeneo hayo kusaka suluhu badala ya kuwatishia na kamatakamata za DCI.