Bunge la kaunti la Nakuru lamtaka Seneta Keroche aache kulidhalilisha

  • | Citizen TV
    316 views

    Katika kaunti ya Nakuru bunge la kaunti hiyo jana lilijadili mswada wa kumtaka seneta wa kaunti hiyo Tabitha Karanja Keroche kukoma kuidalilisha na kudharau bunge hilo. Hii ni baada ya Seneta Keroche mwezi jana kupitia kwa viombo vya habari kulitaka bunge hilo kumung'oa mamlakani Gavana wa kaunti hiyo Susan Kihika kwa kile seneta Keroche alichotaja kama Gavana Kihika kushindwa kutekeleza majukumu yake baada ya mvurutano wa umilik wa hosipitali ya War Memorial, kaunti ya Nakuru ilichukua hosipitali hiyo mwezi jana baada watu saba wakiwemo wakurungenzi watatu kufikiswa mahakamani Nakuru na kushitakiwa kwa madai ya kutumia vyeti ghushi katika kuongeza miaka ya umiliki wa hosipitali hiyo kwa miaka mingine hamsini Zaidi. Alex Mbugua mwakilishi wadi kutoka Lakeview ndiye aliyeleta mswada huo akimtaka spika Maina Karuri wa bunge hiyo pamoja na kiongozi wa wengi kumuandikia seneta barua ya kufika katika bunge hiyo na na kuelezea sababu za kutaka Kihika kuondolewa uongozini. Wanadai Seneta Keroche hakufata Sheria za bunge kwa kwenda bungeni na kuwaelezea sababu za kumuondoa Kihika badala yake alitumia vyombo vya habari na mikutano ya hadara.