Baraza la manaibu gavana lalamikia mikwaruzano kati ya magavana na manaibu

  • | Citizen TV
    744 views

    Baraza la manaibu gavana nchini limelalamikia tofauti zilizopo kati ya manaibu gavana na magavana likisema kuwa mkwaruzano huo unalemaza utoaji wa huduma kwa wananchi. baraza hilo limetaja kaunti za Meru na Kisii kama baadhi ya kaunti zilizokumbwa na misukosuko ya uongozi na kusisitiza umuhimu waushirikiano wa viongozi hao kwani nyadhifa hizo zimeratibiwa na kulindwa na katiba.