Magavana wateta kuhusu kupungua kwa mgao

  • | Citizen TV
    421 views

    Baraza la Magavana limeonyesha wazi kughadhabishwa kwake na serikali kuu kuhusu upungufu wa shilingi bilioni 33 kwenye bajeti ya Ugatuzi katika mwaka wa kifedha wa 2024 -2025. Baraza hilo linateta kuhusu hatua hiyo likisema itahujumu shughuli za kaunti. Hata hivyo, rais William Ruto amewataka magavana kuridhika na fedha zilizotengwa kwani, kuna changamoto ya hali ya uchumi .