Mahakama yaamuru mhubiri tata Mackenzie kutibiwa

  • | Citizen TV
    3,739 views

    Hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa Alex ithuku ameagiza washukiwa wa mauwaji ya shakahola kupelekwa hospitalini kwa matibabu na kufanyiwa uchunguzi zaidi. Hii ni baada ya mhubiri Paul Mackenzie na wenzake 94 kushindwa kuhudhuria kikao cha mahakama kinachojadili hatma ya dhamana yao baada ya kuwasili mahakamani wakiwa wadhaifu. Wakili wao Wycliffe Makasembo alidai kuwawashukiwa hao wameanza tena kufunga kula na kunywa gerezani. Inadaiwa washukiwa hao hawajala kwa siku sita. Iliwalazimu maafisa wa polisi kuwasaidia washukiwa kuwatoa kwenye magari na hata hakimu kuzuru eneo walilotengewa nje baada ya kushindwa kufika kizimbani. Kesi hii itaendelea kwa njia ya mtandao tarehe tano machi.