Wanawake wanaofanya kazi ya kusafirisha na kukaanga Dagaa Zanzibar

  • | BBC Swahili
    2,252 views
    Dagaa wa Zanzibar wamejipatia umaarufu mkubwa maziwa makuu, hususani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kwa wanawake wengi hususani wajasiriamali zao hilo la bahari, limekuwa ni sehemu ya kujitaftia riziki. Lakini kabla ya dagaa hawa kuingia sokoni, wapo wale ambao wanahusika kuwabeba, kuwasafisha na kuwakaanga ili wakidhi kiu ya mlaji. Mwandishi wa BBC Halima Nyanza amewatembelea wanawake wanaofanya shughuli hizo katika kituo kikuu cha kukaushia Dagaa visiwani Zanzibar, na kuelezwa changamoto lukuki wanazokabiliana nazo. . . . . 🎥: Nicholas Mtenga #dagaa #zanzibar #BBCSwahili65